Advertise with us today here...

Reach your market today and expand your network and increase your profit....

Advertise with us today contact us via marketing@olais.co.tz | +255757599666

Vitenge Market

Vitenge Market
Vitenge market place offers you the best and quality vitenge just contact us today

SOWO - Online Market

SOWO - Online Market
Get new and used products online by visit our site everyday hit the link and get subscribed

Saturday, 1 October 2016

MPANGO WA ROOTS & SHOOTS WAZIDI KUTOA ELIMU YA AFYA NA KUJITAMBUA MASHULENI NCHINI TANZANIA.

Mpango wa Mizizi na Chipukizi maarufu kama Roots & Shoots iliyosambaa zaidi ya nchi 140 duniani imezidi kutoa elimu ya afya mashuleni na sasa elimu hii imewafikia zaidi ya wanafunzi 4570 kwa mkoa wa Dar es salaam na mikoa mingine ya Morogoro, Lindi, Mtwara na Pwani.

Awali akizungumza na SOWO Media Ms. Camila J. Roshi amesema “Taasis ya Jane Goodall kupitia mpango wa Roots & Shoots katika mkakati wa kusaidia jamii, vikundi vya Mizizi na Chipukizi kwa upande wa vyuoni umejikita kusaidia watoto wa shule za msingi na sekondari katika kuendeleza uelewa wa masuala yahusuyo afya”

Aliongezea mratibu huyo wa mradi wa Sanitary Hygiene “Katika kipindi hiki taasis imeweza kuwafikia zaidi ya wanafunzi 4570 huku ikionyesha kuwa elimu hii ni vigumu watoto wa kike na wa kiume kuipata katika vipindi vya kawaida madarasani, hivyo sisi tukiwa vijana wa kitanzania tumejipanga kuhakikisha kuwa elimu hii inawafikia watoto wengi zaidi ikiwa tunawafundisha elimu ya kujitambua na afya wawapo shuleni na majumbani”




Watoto wa shule ya sekondari Mnonela Mkoani Mtwara wakionekana katika picha katika darasa la Kujielewa (Self Concept) Mwalimu Camila Roshi hayupo pichani aliendesha mafunzo hayo akiwa ni mratibu wa mradi pia.







Aliendelea “Aidha kwa kuweza kutimiza ndoto za taifa ni lazima kama vijana kusimama kwa pamoja na kuwa wabunifu katika utatuzi wa changamoto zinazotukabili… Katika shule nyingi tulizotembelea zina matatizo ya maji, mazingira na sera ndogo ndogo za mazingira na afya bado hazijapewa kipaumbele”




Mwalimu na Mratibu wa mradi wa Sanitary Hygiene Ms. Camila Roshi akitoa somo kwa wanafunzi jinsi ya kike katika darasa hili wanafunzi walifundishwa usafi wakati na baada ya hedhi na njia za kuepuka kupata maambukizi ya magonjwa yatokanayo na matumizi ya pedi zenye kemikali zinazoweza kuwaletea madhara.




“Sisi vijana wa Tanzania tunapenda kuishauri serikali iweze kutuunga mkono kupitia mradi huu na program ya Roots & Shoots tuweze kutengeneza sera ndogo ndogo za afya, mazingira na elimu na kuweza kupata vijana ambao wanatambua wajibu wao na kuweza kuitetea jamii yao kwa uzalendo wa dhati na moyo wa kujitolea”







Wanafunzi wakionekana pichani na Raisi wa Wentworth African Foundation Bi. Babra Mcbean (Kulia) na Mkufunzi na Mratibu wa mradi wa Sanitary Hygiene Bi. Camila J. Roshi (Kushoto) akikabidhi msaada wa sodo kwa watoto wa kike katika shule ya Mnonela Sekondari Mkoani Mtwara walikabidhi sodo za kuwatosha watoto wa kike kutumia mwaka mzima wa masomo yao wawapo shuleni.








Sambamba na hilo Mratibu wa Roots & Shoots kwa mkoa wa Dar es salaam Ndugu. Olais K. Raphael amesema “Katika kipindi chote hiki sisi vijana kwa pamoja kupitia mpango wa Roots & Shoots tumeweza kuja pamoja na kubuni njia mbadala zinazoweza kuleta mabadiliko chanya na kuweza kusaidia vijana wenzetu ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa wahanga wakubwa kwa kukosa elimu ya kujitegemea na kuelewa dhana ya kujitolea na uzalendo”


“Imani yangu ni kwamba kwa kiasi kikubwa Roots & Shoots imekuwa chachu ya kuweza kuwafanya vijana kuzidi kuwa na ari ya kujitolea na kujali wengine na hasa kuzingatia kuwa na heshima kwa viumbe hai ikiwa wanyama, jamii na mazingira” Alisema Mratubu huyo.


Tukio hili limefadhiliwa na Wentworth African Foundation kwa ushirikiano wa Kays Hyigiene Products na Jane Goodall's Roots & Shoots - Tanzania

Bonyeza kwenye maandishi hapo juu walipotajwa ili kuweza kupata habari zaidi kuwahusu wadau wa mradi huu.