Mpango wa Mizizi na Chipukizi
maarufu kama Roots & Shoots iliyosambaa zaidi ya nchi 140 duniani imezidi
kutoa elimu ya afya mashuleni na sasa elimu hii imewafikia zaidi ya wanafunzi
4570 kwa mkoa wa Dar es salaam na mikoa mingine ya Morogoro, Lindi, Mtwara na Pwani.
Awali akizungumza na SOWO Media
Ms. Camila J. Roshi amesema “Taasis ya Jane Goodall kupitia mpango wa Roots
& Shoots katika mkakati wa kusaidia jamii, vikundi vya Mizizi na Chipukizi
kwa upande wa vyuoni umejikita kusaidia watoto wa shule za msingi na sekondari
katika kuendeleza uelewa wa masuala yahusuyo afya”
Aliongezea mratibu huyo wa mradi
wa Sanitary Hygiene “Katika kipindi hiki taasis imeweza kuwafikia zaidi ya
wanafunzi 4570 huku ikionyesha kuwa elimu hii ni vigumu watoto wa kike na wa
kiume kuipata katika vipindi vya kawaida madarasani, hivyo sisi tukiwa vijana
wa kitanzania tumejipanga kuhakikisha kuwa elimu hii inawafikia watoto wengi
zaidi ikiwa tunawafundisha elimu ya kujitambua na afya wawapo shuleni na
majumbani”
Watoto wa shule ya sekondari Mnonela Mkoani Mtwara wakionekana katika picha katika darasa la Kujielewa (Self Concept) Mwalimu Camila Roshi hayupo pichani aliendesha mafunzo hayo akiwa ni mratibu wa mradi pia.
Aliendelea “Aidha kwa kuweza
kutimiza ndoto za taifa ni lazima kama vijana kusimama kwa pamoja na kuwa
wabunifu katika utatuzi wa changamoto zinazotukabili… Katika shule nyingi
tulizotembelea zina matatizo ya maji, mazingira na sera ndogo ndogo za
mazingira na afya bado hazijapewa kipaumbele”
Mwalimu na Mratibu wa mradi wa Sanitary Hygiene Ms. Camila Roshi akitoa somo kwa wanafunzi jinsi ya kike katika darasa hili wanafunzi walifundishwa usafi wakati na baada ya hedhi na njia za kuepuka kupata maambukizi ya magonjwa yatokanayo na matumizi ya pedi zenye kemikali zinazoweza kuwaletea madhara.
“Sisi vijana wa Tanzania
tunapenda kuishauri serikali iweze kutuunga mkono kupitia mradi huu na program
ya Roots & Shoots tuweze kutengeneza sera ndogo ndogo za afya, mazingira na
elimu na kuweza kupata vijana ambao wanatambua wajibu wao na kuweza kuitetea
jamii yao kwa uzalendo wa dhati na moyo wa kujitolea”
Wanafunzi wakionekana pichani na Raisi wa Wentworth African Foundation Bi. Babra Mcbean (Kulia) na Mkufunzi na Mratibu wa mradi wa Sanitary Hygiene Bi. Camila J. Roshi (Kushoto) akikabidhi msaada wa sodo kwa watoto wa kike katika shule ya Mnonela Sekondari Mkoani Mtwara walikabidhi sodo za kuwatosha watoto wa kike kutumia mwaka mzima wa masomo yao wawapo shuleni.
Sambamba na hilo Mratibu wa Roots
& Shoots kwa mkoa wa Dar es salaam Ndugu. Olais K. Raphael amesema “Katika
kipindi chote hiki sisi vijana kwa pamoja kupitia mpango wa Roots & Shoots
tumeweza kuja pamoja na kubuni njia mbadala zinazoweza kuleta mabadiliko chanya
na kuweza kusaidia vijana wenzetu ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa wahanga
wakubwa kwa kukosa elimu ya kujitegemea na kuelewa dhana ya kujitolea na
uzalendo”
“Imani yangu ni kwamba kwa kiasi
kikubwa Roots & Shoots imekuwa chachu ya kuweza kuwafanya vijana kuzidi
kuwa na ari ya kujitolea na kujali wengine na hasa kuzingatia kuwa na heshima
kwa viumbe hai ikiwa wanyama, jamii na mazingira” Alisema Mratubu huyo.
Tukio hili limefadhiliwa na Wentworth African Foundation kwa ushirikiano wa Kays Hyigiene Products na Jane Goodall's Roots & Shoots - Tanzania
Bonyeza kwenye maandishi hapo juu walipotajwa ili kuweza kupata habari zaidi kuwahusu wadau wa mradi huu.
Taarifa na Olais Youth Educator

No comments:
Post a Comment