![]() |
| Mh. Mizengo Pinda akiwa katika studio za BBC- Swahili hapa mjini Uingereza katika mahojiano na mtangazaji Salim Kikeke (Picha na BBC - Swahili) |
Swali hili limekuwa gumu kwa Mh. Pinda kulijibu ikiwa ni hasa bado kiongozi wa serikali. Ndugu Salim Kikeke aliuliza swali hili akiwa na lengo la kutaka kujua kuwa mchakato wa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umefikiwa wapi watu wakiwa wanasema ya kuwa katiba hii ni ya chama kimoja yaani chama tawala?
Huku Mh. Pinda akijibu swali hili alitoa ufafanuzi mzuri ikiwa ni kwamba katiba ya tume ilipelekwa ndani ya Bunge Maalum la katiba kwa lengo la maboresho na sio kwa lengo la kuipitisha katiba.
Ni jibu zuri na tukumbuke ya kuwa ndio kazi nchi iliyowatuma wabunge hawa kwenda kuifanya na ndio maana kuna kazi mamia zimekwama ikiwa ni lengo la kuhakikisha ya kuwa nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunakuwa na katiba bora na yenye maslahi kwa taifa letu la leo na kesho na kwa vizazi vyote.
Ingia link hii hapa ujionee na kusikia kipande kidogo cha Mh. Pinda kutangaza nia akiwa katika mahojiano na Ndugu. Kikeke katika studio za BBC - Swahili hapa mjini Uingereza.
https://www.facebook.com/video.php?v=509239709213496&set=vb.174247279379409&type=2&theater
Mwandishi wako Olais K. Raphael | Speak Out With Olais - Media

No comments:
Post a Comment