Advertise with us today here...

Reach your market today and expand your network and increase your profit....

Advertise with us today contact us via marketing@olais.co.tz | +255757599666

Vitenge Market

Vitenge Market
Vitenge market place offers you the best and quality vitenge just contact us today

SOWO - Online Market

SOWO - Online Market
Get new and used products online by visit our site everyday hit the link and get subscribed

Monday, 19 December 2011

Riwaya ya "Sauti ya mtoto aliyepotea"

SURA YA KWANZA
Ni mtoto mdogo mwenye umri wa miaka kumi na moja alikuwa anaishi na mama yake hapa kijijini Ntitye mkoani Sago katika nchi ya Naele.
Mtoto huyu alionekana ni msichana mwenye sura nzuri na tabia nzuri ila tatizo ni hali ya umasikini iliyokuwa imetawala katika nchi ya Naele na kufanya familia nyingi kukosa amani na maelewano.
Kwani katika hali nzima ya uchumi wa Naele watu walikosa ari na hamasa ya kufanya shughuli za uzalishaji na elimu ya uzazi wa mpango na pia elimu ya uzalendo katika kujenga nchi bora na yenye amani kwani amani bila uzalendo, uwajibikaji na upendo ni sawa na siasa bila mipango.
Watu wa nchi ya Naele walikuwa wanaendekeza sana suala la starehe na kusahau uzalishaji na mwisho wa siku hakuna anayekubali kupokea lawama na kusingizia watu wengine.
Kwa mfano watu wa Naele wanailaumu sana serikali yao kwa kushindwa kutoa huduma bora lakini wananchi hawa hawapo tayari kufuatilia vikwazo vya maendeleo haya na kuyafanyia kazi matatizo yaliyopo kwa ushirikiano lakini lawama zilielekezwa kwa serikali ya Naele.
Watu wanachangia harusi na kushiriki sherehe zenye garama za mamilioni ya shilingi, lakini wanasahau sana matatizo yanayowaandama ndani ya jamii ya nchi ya Naele.
Katika familia hii ya mtoto Maidze inayopatikana katika kijiji cha Ntitye, familia hii ilionekana kuwa na hali ya maelewano sana ila kwa muelekeo wa hali ya kimaisha na uchumi katika nchi ya Naele familia ya Maidze ilionekana kuyumba sana na kukosa amani.
Kwani mtoto alikuwa na tabia nzuri sana ila tatizo lilikuwa ni kwa wazazi wake Maidze kwa wazazi wote wawili kuwa wanywa pombe maarufu sana katika kijiji hiki cha Ntitye.
“Mjomba, mjomba” Ni maidze alimuona mjomba wake na kumuita kwa sauti ya juu sana huku akimkimbilia.
“Shkamoo mjomba” ni Maidze alisikika kwa sauti ya unyonge akitoa salamu kwa mjomba wake.
“Naam mjomba, haujambo!” Ni mjomba wake Maidze alisikika akiitikia ile sauti ya unyonge kutoka kwa mtoto Maidze.
“Sijambo mjomba”
Maidze alijikaza na kuongea na mjomba wake na moja kwa moja Maidze alisikika akitoa lawama zake kuhusu wazazi wake mbele ya mjomba wake.
“Mjomba samahani, nakuomba unisikilize japo kidogo na unielewe, kuwa namaanisha nini katika maongezi haya” Ni maidze alisikika akijielezea kwa mjomba wake kwa uchungu wa hali ya juu.
“Mjomba nina umri wa miaka kumi na moja sasa lakini wazazi wangu bado hawajanipeleka shule lakini mjomba mimi ninahitaji kwenda kusoma” Mjomba wake Maidze alionekana kuwa mkimya sana kumsikiliza Maidze kwani alikuwa anatoa maelezo mazuri na ya kuhuzunisha kwa wale wazazi wanaopenda maendeleo ya watoto wao.
Maidze alizidi kujieleza kwa mjomba wake huku akiwa anatoa machozi ya hasira na uchungu mwingi kwa kukosa haki yake ya msingi ya kupata elimu na kuondoa ujinga.
“Mjomba mimi ni msichana mdogo sana lakini mama yangu amekuwa akinilazimisha niolewe na watu wakubwa kitu ambacho mimi nimekuwa sihitaji kufanya hata kidogo kama mama yangu alivyokuwa ananitaka.
Je nini kitaendelea baina ya mjomba wake Maidze na Maidze mwenyewe? usikose kufuatilia mkasa huu wa kufundisha na kuelimisha

Msimulizi wako ni Mwandishi Olais K. Raphael

kazi hii ina haki miliki hivyo si ruhusa kwa mtu yeyote kunakili au kuchapisha kazi hii ila ni ruhusa kutoa maoni yako na kama umekipenda kitabu hiki ni ruhusa kuwasiliana na mmiliki kwa email ya kikundi naeleprogram@gmail.com au ya mwandishi olais_raphael@hotmail.com

No comments:

Post a Comment