Advertise with us today here...

Reach your market today and expand your network and increase your profit....

Advertise with us today contact us via marketing@olais.co.tz | +255757599666

Vitenge Market

Vitenge Market
Vitenge market place offers you the best and quality vitenge just contact us today

SOWO - Online Market

SOWO - Online Market
Get new and used products online by visit our site everyday hit the link and get subscribed

Friday, 8 August 2014

Haki za binadamu


Haki za binadamu ni wazo la kuwa kila mtu anastahili haki kadhaa si kwa kutegemea cheo, wala taifa, wala tabaka, wala jinsia, wala dini kwa sababu tu yeye amezaliwa binadamu.
Haki hizi zimeorodheshwa hasa katika Tangazo kilimwengu la haki za binadamu lililotolewa na Umoja wa Mataifa mwaka 1948. Tamko la UM lilikuwa kamilisho la majadiliano kuhusu haki hizi yaliyoendelea kwa karne kadhaa.
Hoja la kimsingi ni kwamba, "Watu wote wamezaliwa huru; hadhi na haki zao ni sawa. Wote wamejaliwa akili na dhamiri, hivyo yawapasa watendeane kindugu". (Kifungu 1 cha tangazo la 1948).
Mizizi ya haki hizo inapatikana katika falsafa na dini mbalimbali ya tangu kale, lakini ilikuwa wakati wa zama za mwangaza tangu karne ya 18 ya kwamba haki hizi zilijadiliwa kwa undani pamoja na swali: ni matokeo gani kuwepo kwa haki hizi yanaleta kwa utaratibu wa siasaserikali na jamii.

Mfano wa haki za kimsingi

Haki za binadamu za kimsingi ni pamoja na:

  • Kuishi
  • Kuchagua kazi - kutokuwa mtumwa
  • Kuwa na mali
  • Kutoa maoni yake kwa uhuru
  • Kuwa salama, kutotishwa
  • Kuwa na kinga dhidi ya hatua za kisheria, pamoja na nafasi ya kupinga kwa njia halali
  • Kutokamatwa kwa kosa la mtu mwingine
  • Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya mahakama
  • Kutazamiwa kuwa bila ya hatia kabla mahakama haijatoa hukumu
  • Kuwa na uraia wa nchi fulani
  • Kupiga kura katika uchaguzi huru
  • Kupewa kimbilio kama nchi asilia inazuia uhuru wa msingi
  • Kuchagua dini na kuishi kufuatana na dini
  • Kupinga pamoja na wengine maazimio ya serikali kwa njia ya amani
  • Kupata elimu
  • Kufunga ndoa na mtu mzima yeyote
Kwa mengine angalia makala juu ya tangazo kilimwengu la haki za binadamu.

Ingia hapa chini ujionee Tangazo la Haki za Binadamu mwaka 1945

Shirika zinazopigania haki za binadamu[hariri | hariri chanzo]


Chanzo chetu; http://sw.wikipedia.org/wiki/Haki_za_binadamu

No comments:

Post a Comment