Wabunge 16 wanaowindwa

ORODHA ya majina ya wabunge 16
wanaotafutwa ili Bunge Maalumu la
Katiba (BMK) liweze kutimiza akidi
ya wapiga kura watakaoweza kupitisha
Katiba imepatikana. Wabunge hao ni
sehemu ya wabunge 67 kutoka Zanzibar
walio miongoni mwa wabunge 201
walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kujiunga na BMK wakitoka katika taasisi
mbalimbali.
Raia Mwema limeelezwa na vyanzo vyake kutoka ndani ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na BMK kwamba wabunge hao 16 ndiyo watakaofuatwa na
kama watahudhuria na kupiga kura katika vikao halali, Rasimu ya Katiba
iliyotayarishwa na Tume ya Jaji Warioba itaweza kupitishwa na hatimaye
kupelekwa kwa wananchi ili ipigiwe kura.
“Kazi tumemaliza sasa. UKAWA waje au wasije BMK litakaa na kumaliza
kazi yake iliyotumwa na Watanzania. Majina ya wabunge ambao tunaweza
kuwapata yapo tayari, Raia Mwema limeambiwa na moja ya vyanzo vyake
vya kuaminika juzi Jumatatu.
Majina ambayo gazeti hili limepewa ni la Yasmine Aluu, Yusuf Omar Chunda,
Asha Makungu Othman, Siti Abasi Ali, Thuwein Issa Thuwein, Sheikh Nassor
Mohamed Ibrahim, Louis Majaliwa na Abdallah Abbas Omar.
Majina mengine ya wajumbe hao kutoka Zanzibar walio katika BMK
wanaotarajiwa kushawishiwa kuendelea na Bunge ni Biubwa Yahya Othman,
Fatma Mohamed Hassan, Sheikh Thabit Jongo, Adilla Hilal Vuai, Tatu Mabruk
Haji, Waziri Rajab, Vuai Ali Vuai na Fat-Hiya Zaharani Salum.
Wajumbe hao, gazeti hili limeelezwa, watafuatwa kutokana na vigezo
walivyonavyo ambavyo baadhi vimetajwa kuwa ni kuwa wana CCM, watu
kutoka katika familia zilizoshiriki katika Mapinduzi ya mwaka 1964 na wengine
ni wale wanaelezwa kwa “kuwa wasikivu.”
Kazi ya kuzungumza na wabunge hao inasimamiwa na mmoja wa
wabunge mashuhuri kutoka visiwani Zanzibar ambaye anaruhusiwa
kutumia pia watu wengine kuongeza ushawishi.
Ili kupitisha Katiba mpya, BMK linatakiwa kupiga kura kwa zaidi ya
theluthi mbili ya wabunge wake wa Bara na Zanzibar; lakini wakati
CCM ina uhakika wa kupata theluthi mbili Bara, inahitaji wabunge hao
16 ili kupata theluthi mbili ya wabunge wa Zanzibar.
Baadhi ya wabunge wa BMK kama vile Profesa Abdallah Safari,
wanapinga suala hilo la kutafuta idadi hiyo ya wabunge pasipo kwanza
kuwapo kwa maelewano baina ya UKAWA na CCM.
Hata hivyo, gazeti hili limeelezwa kwamba kuna uwezekano wa
kupata wabunge zaidi ya hao 16 kutoka Zanzibar, mara baada ya
kufanyika kwa kikao cha Mkutano wa Maridhiano uliopangwa
kufanyika mwishoni mwa wiki hii mjini Dodoma na kuhudhuriwa
na Kikwete pamoja na marais wastaafu wa Tanzania.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba,
ameeleza hofu yake kwamba endapo Bunge litalazimishwa kuendelea,
huenda wabunge wa UKAWA wakaenda bungeni kwa minajili ya kupata
posho pekee na si kwa ajili ya kupata Katiba.

“Kabla halijaahirishwa, BMK lilitumia shilingi bilioni saba. Maana yake
linaweza kutumia tena kiasi kama hicho kwa kulipa watu ambao
hawatakuwa na nia ya kutafuta Katiba bali kupata posho na kututia
hasara pasipo sababu”, alisema Kibamba katika mazungumzo yake na
gazeti hili.

CHANZO; RAIA MWEMA
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/wabunge-16-wanaowindwa#sthash.N0QNBbFv.dpuf
No comments:
Post a Comment